Serikali ya Awamu ya Nane Zanzibar yaeleza dhamira yake ya kukuza uchumi wake kupitia sekta ya Viwanda

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla alitoa kauli hiyo wakati alipofanya ziara ya kukagua eneo maalum la Viwanda vidogo vidogo liliopo Amani Mkoa wa Mjini Magharibi. Alisema serikali ya awamu ya nane chini ya uongozi wa Dk. Hussein Ali Mwinyi imeamua kuweka mkazo katika Sekta ya uwekezaji kwa kuwakaribisha wawekezaji